Nape Nnauye awatuhumu UKAWA kwa kutengeneza kadi bandia za CCM na kuzigawa
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, amedai kuwa chama hicho kimebaini mchezo mchafu unaotaka kufanywa na UKAWA wa kutengeneza kadi bandia za chama hicho na kuzigawa kwa watu wao, ili baadaye asipopita mgombea wao, ionekane wana CCM wanakihama chama kwa kurudisha kadi zao.
Akizungumza katika Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana, Nape alisema kuna taarifa za uhakika kuwa kuna baadhi ya makundi ya UKAWA yamepanga mchezo huo wa kutengeza kadi bandia.
Akizungumza katika Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana, Nape alisema kuna taarifa za uhakika kuwa kuna baadhi ya makundi ya UKAWA yamepanga mchezo huo wa kutengeza kadi bandia.
“Wameanza kuratibu mchezo huo ili wazigawe kadi hizo kwa watu wao, ili baadaye asipopita mgombea wao, ionekane wana CCM wanakihama chama chao kwa kurudisha kadi hizo kwenye shughuli mbalimbali za vyama hivyo vinavyounda Ukawa.
“Wakati tunachunguza kwa kina suala hilo, Ukawa waache mchezo huo wa ovyo na Watanzania wakwepe mchezo huo na wawe makini,” alisema
“Wakati tunachunguza kwa kina suala hilo, Ukawa waache mchezo huo wa ovyo na Watanzania wakwepe mchezo huo na wawe makini,” alisema
No comments