CCM wasema: Kuondoka kwa Slaa, Lipumba, Zitto UKAWA watanyooka tu....
Watanyooka tu! Hiyo ndiyo kauli waliyoitoa wafuasi wa CCM jijini Dar baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (Cuf), Ibrahim Lipumba kujiweka pembeni katika shughuli za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Slaa amedaiwa kujichimbia nyumbani kwake Mbweni jijini Dar na kukataa kuzungumzia hatma yake kisiasa na kuacha shughuli za Ukawa zikiendelea bila uwepo wake huku Agosti 6, mwaka huu, Lipumba akijitokeza hadharani na kutangaza kujivua wadhifa wake akidai kwa kile alichodai kukiukwa kwa makubaliano ya awali ya umoja huo.

Mara baada ya vigogo hao kujiweka pembeni, wanachama mbalimbali wa CCM walizungumza na Risasi Jumamosi na kueleza hisia zao juu ya viongozi hao na kusema kujitoa kwao ni ishara nzuri ya umoja huo kusambaratika.
“Ukawa watanyooka tu. Sisi tulijua zamani kwamba safari yao waliyoianzisha haiwezi kufanikiwa, ona sasa Slaa ameshajiweka pembeni, hashiriki vikao vya Ukawa, Lipumba naye ndiyo huyo ameshajivua uongozi.
“Sasa kama mwenyekiti wa chama anajivua uongozi ikiwa imebaki miezi miwili tu kuelekea uchaguzi kuna nini hapo? Tayari wamekaa, CCM ushindi mapemaaa,” alisema Gilbert, mkazi wa Sinza jijini Dar.
Kama hiyo haitoshi, Mary wa Ubungo jijini Dar, alisema:
“Ukawa wanaangukia pua. Siku si nyingi tutasikia wametibuana na kurejea kulekule kwa kila chama kusimamisha mgombea wake.”

No comments