Watu 4 wafariki na wengine 11 wajeruiwa vibaya katika ajali mkoani Kilimanjaro
Watu 4 wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya Fuso iliyokuwa imebeba mchele kugonga haice iliyokuwa imebeba abiria kwa nyuma katika eneo la daraja la mto Kikavu wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Fulgence Ngonyani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha gari aina ya haice iliyokuwa imebeba abiria ikitokea Sanya juu kuelekea mjini Moshi na fuso hiyo iliyokuwa imebeba mchele ikitokea mkoani Shinyanga kuelekea mjini Moshi.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba dereva wa Fuso ambaye hajafahamika jina lake ametoroka baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kwamba eneo hilo ambalo ajali hiyo imetokea kuna mteremko mkali.

Baadhi ya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kwa matibabu na badhi ya mashuhuda wameelezea chanzo cha ajali hiyo kuwa uzembe wa dereva wa gari aina ya Fuso kuendesha gari kwa mwendo kasi katika eneo hilo ambalo lina vielelezo vinavyoonyesha eneo hilo ni hatari.
Kwa upande wake mganga mkuu idara ya mapokezi katika hospitali ya rufaa ya KCMC Dk Noel Makundi amesema jumla ya majeruhi saba waliofikishwa katika hospitali hiyo majeruhi wanne hali zao ni mbaya zaidi.
Ajali hiyo ambayo imetokea majira ya saa 12.40 asubuhi imesababisha foleni ndefu kutokana na magari kushindwa kuendelea na safari kwa zaidi ya saa tano.

No comments