Header Ads

Ray C: Nimenenepa Lakini Kiuno Bila Mfupa Kipo Pale Pale, “Sina tofauti na Ray C wa zamani”



Rehema Chalamila aka Ray C amewatoa hofu mashabiki wa muziki wake, kuwa unene wake haujakiathiri kiuno chake bila mfupa bali kimemwongezea uwezo wa kukatika kuliko zamani!

Ray C ambaye alitamba na nyimbo kama ‘Sikuhitaji’ na ‘Umeniacha’, ameiambia Global TV kuwa anahisi uwezo wake wa kukatika umeongezeka zadii kutokana na unene.

“Sina tofauti na Ray C wa zamani,” alisema. Ray C ni yule yule, kiuno cha zamani ni kile kile. Sema sasa hivi kina nyama kidogo kwahiyo sasa hivi nikifanya kidogo tu yaani ni rahisi zaidi kwangu.”

No comments

Powered by Blogger.