Chumbani zaidi!!!! Acha haraka jifunze kuwa na subhira...
Nianze kwa kuwatakia siku njema kabisa ya Alhamisi disemba 4, ikiwa ni ishara kwamba mwisho wa mwaka unakaribia. Ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba tumekuwa miongoni mwa waliochaguliwa kuuona mwezi huu, ingawa yatupasa tuombe sana ili tuumalize. Maana mnajua kwa kiasi gani wapendwa wetu walivyopotea na hatutawaona tena.
Mada yangu leo kama unavyoweza kuiona hapo juu kwenye kichwa chake cha habari, inawazungumzia zaidi akina dada, kwa sababu zilizo wazi kabisa kwamba, wao ndiyo maua ya dunia, bila wenyewe hata maisha sijui yangekuwaje.
Ni jambo la kweli kwamba mara nyingi wanaume ndiyo wanaokuwa wa kwanza kutangaza nia kwa mwanamke tofauti na inavyokuwa kinyume chake. Inapotokea mwanamke ‘anamtokea’ mwanaume, huwa ni gumzo na siyo ajabu kukuta mwanaume akikataa, anaona kama vile anategewa au mwanamke anayemtongoza ana kasoro.
Kwa wanaume, wengi wao hupenda baada ya kukubaliwa katika kutongoza kwao, kinachofuata kiwe ni tendo la ndoa na si vinginevyo wakati kwa wanawake, baada ya kukubaliwa, wao hupenda kwanza wazoeane kwa maongezi, vijizawadi na mitoko ya hapa na pale kabla ya kuhitimisha kwa tendo.
Hii ni hulka ambayo imeendelea hadi kujenga mazoea, kiasi kwamba wanaume wakimpata mwanamke wa kushiriki naye tendo siku ya kwanza tu ya kukutana kwao, huwaona kama wasiofaa. Wamezoea wakikubaliwa, wazungushwe japo siku mbili tatu kabla ya kumalizana.
Sasa utamu unakuja pale mwanaume baada ya kukubaliwa, kwa kawaida, atatoa mwaliko kwa mwenzake kwa ajili ya mazungumzo, mara nyingi huwa ni hotelini kwa ajili ya chakula cha mchana au kwa wanywaji basi hukutana eneo zuri kwa ajili ya kujipatia mbili tatu.
Inaweza kuwa siku ya kwanza, ya pili na pengine kwa siku kadhaa. Katika kipindi hicho, mwanaume atakuwa ametoa ofa kama hivyo ya vinywaji, vocha na hata pesa kwa mwenza wake. Uzoefu unaonyesha kuwa mara nyingi wakaka wanapoulizia kuhusu faragha, hukutana na maswali au majibu kama “yaani mbona wewe una haraka? Harakaharaka haina Baraka”.
Na hata wengine huwaambia maneno kama “Yaani wewe hicho ndicho unachokiwaza.” Kauli hizi za akina dada huwa na nia ya kupunguza spidi ya jamaa wenye uchu. Kama nilivyodokeza pale juu, kwa mujibu wa mazoea yaliyojengeka, inatarajiwa kuwa walio katika uhusiano watachukua muda kidogo kabla ya kufikia hatua ya kushiriki tendo.
Lakini wakati akina dada wamekuwa wakisisitiza kutokuwa na haraka ya kushiriki tendo kwenye uhusiano mpya, uzoefu pia unaonyesha wao huwa hawasubiri kabla ya kuanza mambo yao. Katika siku ya kwanza ya kutongozwa na kukubali, kesho yake wataanza kuomba vocha.
“Baby naomba vocha niongee na mama, yaani nimemmiss sana,” utasikia msichana akimwambia mpenzi wake. Baadhi ununua muda wa maongezi kweli, lakini wengi wao huchuma hela kutegemea na uzuri wa mdada.
“Baby naomba niongezee elfu ishirini kuna kitu nataka kununua hapa nitakurudishia..” wengine huja na kauli kama hizi. Kifupi ni kwamba wasichana wengi huwasumbua wenza wao wapya kwa staili kama hii. Maombi kama haya huwafanya wanaume wahangaike sana kuwatimizia wapenzi wao, lakini pia huwaumiza sana kisaikolojia.
“Hivi kama huyu anaanza kupiga mizinga hata hatujafahamiana vizuri, hivi akishakuwa mpenzi wangu si ndo balaa,” baadhi ya akina kaka hujiuliza. Na hivyo kujikuta wakibaki njia panda wacjue la kufanya na hatimae wanaachana au kuzaraulia kwa mambo ya haraka haraka ya siyo kuwa na maana.

No comments