BREAAKING NEWSSS....MAHAFALI YA PILI YA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA Mgeni rasmi ni Mh. Prof. Mark Mwandosya
Utangulizi....Wahitimu na wanataaluma pamoja na mkuu wa chuo waliingia kwa maandamano yaliyojaa nakshinakshi na nyuso zenye furaha kuonyesha umuhimu wa tukio hili kwa wote wanaohitimu pamoja na wasindikizaji(washehereshaji), Sherehe hii ambayo inafanyika katika ukumbi wa Nyerere hall wa chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya,Mwenyekiti wa baraza la chuo pamoja na Makamu wa chuo waliongoza maandamano hayo na kuwakaribisha wahitimu wote wa mahafali hii ya pili tangu kuwa chuo kikuu.
Makamu mkuu wa chuo Prof. J Msambichaka alimuomba Mwenyekiti wa baraza la chuo Prof. Penina Mlama amkaribishe Mkuu wa chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Prof. Mark Mwandosya (Mb) kufungua rasmi sherehe ya mahafali:
Na baada ya hapo alimuomba Mwenyekiti wa baraza la chuo Prof. Penina amkaribishe Mheshimiwa Mkuu wa Chuo Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Mh. Prof. Mark Mwandosya (Mb), "Ndugu mkuu wa chuo kwa niaba ya Baraza la Chuo,Wafanyakazi na wanafunzi wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya nakuomba ufungue rasmi mahafali ya pili ya Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya leo Tarehe 20 mwezi 12 mwaka 2014. Karibu sana" alisema Prof. Penina Mlama.
Mheshimiwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Mh. Prof. Mark Mwandosya akatangaza rasmi kufunguliwa kwa mahafali ya pili ya Chuo." KWA MAMLAKA NILIYOPEWA NATANGAZA KWAMBA MAHAFALI YA PILI YA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA YAMEFUNGULIWA RASMI" alisema Prof. M Mwandosya.
Mheshimiwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Mh. Prof. Mark Mwandosya akatangaza rasmi kufunguliwa kwa mahafali ya pili ya Chuo." KWA MAMLAKA NILIYOPEWA NATANGAZA KWAMBA MAHAFALI YA PILI YA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA YAMEFUNGULIWA RASMI" alisema Prof. M Mwandosya.
Baada ya kufunguliwa kwa Mahafali na Mh. mkuu wa chuo kilichofuata ni utambulisho wa wageni waalikwa katika mahafali hii Akiwamo Mke wa Prof. Mwandosya pamoja na watoto na ndugu wengine walioudhuria mahafali hii ya pili ya chuo kikuu cha sayansi na teknolojia mbeya.
Katika changamoto za wahitimu walizo kutana nazo waliziorozesha katika risala yao na kufafanuliwa(kutolewa maelezo kwa ufupi na makamu mkuu wa chuo katika Risala yake na baada ya hapo ilikabidhiwa kwa Mkuu wa chuo na Pro. J Msambichaka ambaye ndiye aliyeisoma risala hiyo.
Katika changamoto za wahitimu walizo kutana nazo waliziorozesha katika risala yao na kufafanuliwa(kutolewa maelezo kwa ufupi na makamu mkuu wa chuo katika Risala yake na baada ya hapo ilikabidhiwa kwa Mkuu wa chuo na Pro. J Msambichaka ambaye ndiye aliyeisoma risala hiyo.
Kutunuku Vyeti...
Mshereheshaji alimkaribisha Makamu mkuu wa chuo aliemkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Chuo(Prof. Penina) iliamkaribishe mkuu wa chuo kuwatunuku wahitimu wa mahafali Vyeti.....
Prof Penina Mlama " Mheshimiwa Mkuu wa Chuo, Nakuomba uwatuniku wahitimu wetu 1068, VYETI vya Stashahada ya kawaida wahitimu 821 na wahitimu 246 Shahada ya kwanza".
Katika Mahafali haya pia kuna wanafunzi waliofanya vizuri kabisa katika Idara zote na hivyo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Osmund Kaunde aliwasilisha majina ya wahitimu 16 walifanya vizuri zaidi katika fani mbalimbali na kuomba watunukiwe vyeti na zawadi ....
Wanafunzi Bora wa Idara
A) STASHAHADA YA KWANZA
1 Idara ya usanifu majengo Mwanafunzi bora ni Denes G. Njamasi
2 Idara ya Uhandisi Ujenzi " " ni Abuu A. Imoro
3 Idara ya Uhandisi Kompyuta ni Raymond E. kileo
4 Idara ya Uhandisi Umeme na Elektroniki ni Japhet Luchangula
5 Idara ya Uhandisi Mitambo ni Samson M Kilindu
6 Idara ya sayansi na biashara
(a) Teknolojia ya Maabara ni Zena Mwangonela,E
(b) Utawala wa biashara ni Abraham Sinda
B) SHAHADA YA KWANZA
1 Idara ya usanifu majengo Blasius Venance
2 Idara ya Uhandisi Ujenzi Yohana Daudi
3 Idara ya Uhandisi Umeme na Elektroniki Ernest Sollo
4 Idara ya Uhandisi Mitambo Nyanda Madili
5 Idara ya sayansi na biashara Nassoro H. Rubanga
Kundi lingine lilikuwa ni lawanafunzi bora kuliko wote wa chuo
-Japhet Luchangula Wastashahada ya kawaida (idara ya Uhandisi Umeme na Elektroniki)
- Yohana Daudi Washahada ya kwanza(Idara ya Uhandisi Ujenzi)
Kundi la mwisho ni la wanafunzi bora wa kike
-Zena Mwangonela,E Wastashahada ya kawaida (Idara ya sayansi na biashara)
-Chaya Mbozi Washahada ya kwanza(Idara ya Uhandisi Mitambo)
Baada ya kutunukiwa vyeti na zawadi kwa wanafunzi(wahitimu) waliofanya vizuri. Naibu Makamu mkuu wa Chuo cha Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Osmund Kaunde Aliwaita wakuu wa Idara kuwahudhurisha wahitimu wa idara zao waweze kutunukiwa Shahada na Mkuu wa Chuo.
Mkuu wa koleji ya Uhandisi na Teknolojia
A) SHAHADA YA KWANZA
Shahada ya kwanza ya usanifu majengo waliohitimu ni wanafunzi 17 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Shahada ya kwanza ya Uhandisi Ujenzi waliohitimu ni wanafunzi 80 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Shahada ya kwanza ya Uhandisi Umeme waliohitimu ni wanafunzi 54 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Shahada ya kwanza ya Uhandisi Mitambo waliohitimu ni wanafunzi 31 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Shahada ya kwanza ya Uongozi wa biashara waliohitimu ni wanafunzi 64 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Baada ya kutunukiwa vyeti, wanafunzi(wahitimu) wa SHAHADA YA KWANZA, Naibu Makamu mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Osmund Kaunde Aliwaita tena wakuu wa Idara kuwahudhurisha wahitimu wa idara zao waweze kutunukiwa Stashahada na Mkuu wa Chuo.
B) STASHAHADA YA KWANZA
Stashahada ya kwanza ya usanifu majengo waliohitimu ni wanafunzi 57 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Stashahada ya kwanza ya Uhandisi Ujenzi waliohitimu ni wanafunzi 188 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Stashahada ya kwanza ya Uhandisi Umeme waliohitimu ni wanafunzi 166 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Stashahada ya kwanza ya Uhandisi Mitambo waliohitimu ni wanafunzi 120 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Stashahada ya kwanza ya Teknolojia na Mahabara waliohitimu ni wanafunzi 115 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Stashahada ya kwanza ya uhandisi kompyuta waliohitimu ni wanafunzi 91 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Stashahada ya kwanza ya Utawala wa Biashara waliohitimu ni wanafunzi 84 katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Mkuu wa chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kwa MAMLAKA aliyopewa aliwatunuku wahitimu wote wa idara zote za Shahada ya kwanza na Stashahada vyeti vyao kulingana na idara zao.
Nakisha wahitimu wote walipita mbele na kumshika mkono mkuu wa chuo na kupongezana na walimu wao kwa furaha ya kuhitimu kulingana na level zao.
Baada ya tukio la ugawaji wa vyeti kuisha mwenyekiti wa Baraza la Chuo alimuita na kumuomba Mkuu wa chuo avunje au ahitimishe sherehe hizi za Maafali ya pili ya Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.
"KWA MAMLAKA NILIYOPEWA, SASA NAVUNJA RASMI MAHAFALI HAYA YA PILI YA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA". Alisema mkuu wa chuo Prof. M. Mwandosya.
Maandamano ya wanachuo,wahitimu pamoja na mgeni rasmi kuelekea Ukumbini kwaajili ya maafali kuanza.
Baadhi wa wahitimu wa idara mbalimbali wakipiga picha ya pamoja kwaajili ya kumbukumbu.
Idara mbalimbali zikionyesha baadhi ya ujuzi wa kazi za mikono yao kwa Mgeni Rasmi Prof. M Mwandosya ,Ambapo katika Maonyesho haya Mh. aliuliza maswali na kupewa majibu yenye ufasaha kabisa kutoka kwa wahusika wakila Idara.
Wakina Dada taifa la Kesho,Baadhi wa wanafunzi wa Mbeya University of science na technology nao hawakuwa nyuma kuuliza maswali katika maonyesho hayo.
Wakinadada walio hitimu Mahafali ya leo.
Katika mahafali hii pia kulikuwa na Rais mtarajiwa wa Mbeya university of science and technology akiteta Maneno mawili matatu na mama hapo.
Idara ya mapokeze wakiwa katika utanashati wao.
Wadau wengine waliokuwa katika mahafali hii na Mgeni Rasmi alipokuwa anawasili Mh.Prof. Mark Mwandosya.
Asante kwa kutembelea ukurasa wetu huu wa www.paparaziwetu.blogspot.com, Endelea kuwa nasi kwa habari na matukio zaidi.Pia kama bado uja-like page yetu like ilikuhabarika kwa wakati www.facebook.com/paparaziwetu.
ASANTE NA KARIBU TENA
ASANTE NA KARIBU TENA
nzuri saana
ReplyDeleteAsante mama, Ni kazi ya mikono yetu na tunajivunia kuwa na wadau wenye upendo kama wewe
Delete