Header Ads

Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni wezi wa mifugo kuchomwa moto wilayani iramba.

Watu wanne wanao sadikiwa kuwa wezi wa ng’ombe wameuawa na watu wenye hasira kali, kwa kupigwa  na kuchomwa moto katika kijiji cha sheluhi wilayani iramba, baada ya kukutwa wakiwa wamewachinja ngo’mbe hao.

Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo  mwenye kiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya iramba ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Bwana Yahaya Nawanda amewataka wananchi wanapowakamata wahalifu kuacha vitendo vya kujichukulia hatua  za kuwauwa kwa kufanya hivyo wanakuwa hawalisaidii jeshi lapolisi.
Kwa upande wake mama wa mmoja wa marehemu  pamoja na mashuhuda wamesema kitendo cha  mauaji yaliyo fanywa na  wananchi wenye hasira kali wakiwa zaidi ya sabini,hawa kufanya jambo la busara kwani  wange pelekwa kwenye vyombo vya sheria.

Vitendo vya wananchi kuamua kuwauwa wahalifu katika wilaya ya iramba vimekuwa vikishamiri  jambo ambalo siyo sahihi  kwani  wamekuwa wakipoteza ushahidi na kupatikana kwa wahalifu wengine.

No comments

Powered by Blogger.