Ripoti ya CAG kuhusu akaunti ya Escrow yawakilishwa Bungeni
Mwenyekiti
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe
akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya
ESCROW Bungeni Mjini Dodoma leo.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua
jambo wakati akiendesha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakimsikiliza Mhe. Zitto Kabwe (hayupo pichani) wakati akisoma ripoti ya CAG.
Waheshimiwa
Wabunge wakipitia ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto
Kabwe.
Baadhi ya waandishi wanaoripoti habari za Bunge wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu katibu wa Bunge, John Joel akijadiliana jambo na Mhe. Spika Anna Makinda.
Wabunge wakiwa wamesimama kuashiria kuunga mkono taarifa iliyosomwa Bungeni leo na Mhe. Zitto Kabwe.
Mhe Said Arfi akimpongeza Mhe.Zitto Kabwe ,mara Baada ya kumaliza kusoma ripoti ya GAG.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe DEO Filikunjombe akiwasilisha maazimio ya kamati yake.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akitoka
ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirisha Bunge mpaka kesho
ambapo Serikali inatarajiwa kutoa majibu.
No comments