Header Ads

Waumini waleta vurugu kanisani wakimtuhumu askofu kuwa ni freemasons

Waumini wa kanisa la Anglikana Wilaya ya Nyamagana Mwanza walisimamisha kwa muda shughuli za ibada kanisani hapo baada ya kutokea vurugu kubwa.

 Vurugu hizo zilitokea baada ya baadhi ya waumini hao kumtuhumu Askofu wa kanisa hilo Boniface Kwangu kwamba ni mmoja wa wafuasi wa kundi la Freemasons na hufanya kazi za kundi hilo.
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo Shadrack Lazaro alitoa tamko la jinsi askofu wao anavyofanya kazi na kundi la Freemason ndipo waumini walipomvamia na kumtoa nje ya kanisa kwa nguvu na kusababisha vurugu kubwa.

Muumini huyo alisema pamoja na sababu kadhaa za kumkataa askofu huyo pia hawaridhishwi na tabia yake ikiwemo kutaka kubomoa sakafu akidai kuna irizi imefichwa na baadhi ya  waumini wake kanisani hapo

No comments

Powered by Blogger.