Header Ads

MAJERUHI WA AJALI YA LORI LA MAFUTA MBAGALA WAZIDI KUFARIKI DUNIA

Idadi ya watu waliokufa kufuatia ajali ya moto iliyotokana na kulipuka kwa tanki la mafuta la lori lililopinduka Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam imeongezeka hadi kufikia saba.
Aidha, hali za majeruhi tisa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ni mbaya.
Idadi ya vifo imeongezeka baada ya majeruhi waliokuwa wamelazwa MNH wawili kufariki dunia usiku wa kuamkia jana.
Afisa habari Msaididizi wa MNH, Doris Ishenda, alithibitisha kufariki kwa watu hao Nurdin Mazinga (22) na Abas Hugangar, wakazi wa Mbagala.

“Usiku wa kuamkia Jumanne tulipokea majeruhi 15 kutoka Hospitali ya Temeke ambao kati yao sita wameshafariki dunia,” alisema na kuongeza kuwa miili yao imehifadhiwa hospitalini hapo.

Watu 20 waliungua vibaya sehemu mbalimbali za miili na mmoja kufariki dunia papo hapo baada ya kulipukiwa na petroli wakati kundi la vijana walipokuwa wakijaribu kupora mafuta kwenye lori hilo lilopinduka eneo la Mbagala Rangi tatu jijini Dar es Salaam Jumatatu wiki hii usiku.

No comments

Powered by Blogger.