Header Ads

Watu wanne wapoteza maisha katika Ajali nyingine mbaya iliyotokea Gairo mchana wa leo

Ajali nyingine mbaya:Basi la Abiria linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam - Tabora limepata ajali mbaya sana mchana leo katika eneo la  Kiegeya,Gairo na kupelekea zaidi ya watu wanne kupoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana.

Ni majonzi makubwa yametawala katika eneo hilo,huku juhudi za kuokoa miili na majeruhi zikiendelea.ni siku tatu tu zimepita toka ajali nyingine mbaya itokee huko Musoma na kupoteza maisha ya zaidi ya Watanzania 35.

No comments

Powered by Blogger.