Header Ads

Mbunge wa Tabora Mjini Ismail Rage amepata ajali akiwanjiani kuelekea Dodoma

 RAIS mstaafu wa klabu bya Simba sc, ambaye ni mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage imelazwa Hospitali ya mkoa wa Dodoma baada ya kupata ajali ya gari akitokea Tabora kueleka mjini Dodoma leo.

Imeelezwa kuwa Rage alikuwa anakwenda Dodoma kuhudhuria vikao maalumu vya bunge la katiba.Ajali hiyo imetokea eneo la Chigongwe mkoani Dodoma.

Imeripotiwa kuwa katika gari hilo, Mheshimiwa Rage alikuwa na abiria wengine ambao ni mbunge wa viti maalumu,  Munde Tambwe, Issa Chimwaga , Mwanahamisi Ramadhani na Dereva  John NKoya.

Abiria wote walipata majeruhi, isipokuwa dereva wa gari hilo, lakini wanaendelea kupata matibabu na hali zao zinakwenda vizuri.

Rage amezungumza akiwa wodini mkoani Dodoma, na kueleza kuwa amepata majeraha katika bega la mkono wa kushoto na eneo la nyuma ya mgongo.

Rage aliongeza kuwa ajali hiyo imetokea wakati dereva wa gari lao akijaribu kulipita roli, lakini ghafla dareva wa Roli hilo akaingia katikati ya barabara na ikamlazimu dereva wao kwenda pembeni ya barabara na gari kupinduka na kutumbukia kwenye korongo.
Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) Ismail Aden Rage, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, akiwa amelazwa kwenye hospitali ya Rufaa, Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014. Rage alipata ajali eneo la Chigongwe, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, wakati akielekea mjini humo tayari kushiriki vikao vya Bunge Maalum vinavyoanza Jumanne Agosti 5, 2014
Mbunge wa Sikonge mkoani Tabora kupitia CCM, ambaye pia ni Mujumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Said Nkumba, akimjulia hali Rage, hospitalini mjini Dodoma, Jumatatu Agosti 4, 2014

No comments

Powered by Blogger.