Adhabu za aina nne ambazo baraza la Madaktari linaweza kuzitoa kwa IMTU
Baraza la Madaktari Tanganyika (TMC) limesema linasubiri majibu ya ripoti zilizoundwa kuchunguza sakata la utupaji holela wa viungo vya binadamu, kabla ya kutoa adhabu stahiki kwa madaktari waliohusika.
Msajili wa baraza hilo, Peter Luena alisema ingawa ofisi yake haina mamlaka ya kukichukulia hatua za kinidhamu Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na
Teknolojia (IMTU) kinachodaiwa kutupa viungo hivyo, inao uwezo wa kutoa adhabu za aina nne kwa madaktari watakaobainika kuhusika.

Wiki iliyopita Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi waliunda timu mbili tofauti kuchunguza namna ambavyo viungo vya binadamu kutoka IMTU vilivyotupwa katika Bonde la Mto Mpiji, jijini Dar es Salaam.
Luena alisema maadili ya udaktari yanaeleza kuwa iwapo daktari amekiuka taratibu za kazi ataitwa mbele ya Baraza la Madaktari na kusomewa mashtaka yake.
“Iwapo atapatikana na kosa, sheria yetu ina hatua nne za adhabu; onyo la kawaida, karipio kali, kusimamisha usajili wa daktari husika na kama ni kosa kubwa anafutiwa usajili kabisa,” alisema.
Hata hivyo, alisema daktari atakayepewa adhabu anaweza kujitetea na kuomba apunguziwe adhabu husika, akikataliwa anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania.

No comments