Je wajua?..Pamoja na Tanzania kuwa ni nchi ya pili kwa vivutio vya utalii bado kuna huduma duni za utalii.
Pamoja na Tanzania kuwa ni nchi ya pili kwa vivutio vya utalii duniani baada ya nchi ya Brazil lakini bado ipo nyuma kwa utoaji wa huduma za utalii ikiwa ni nchi ya mia moja na kumi kati ya nchi mia moja na thelasini na tatu hali inayoweza changia kupunguza pato la taifa ilinalotoka na sekta ya utalii.
Kufuatia hali hiyo wadau wa sekta ya utalii kutoka mkoa wa Arusha wametakiwa kuandaa mikakati malu ya kuinua kiwango cha utoaji wa huduma za utalii kwa kukiongezea uwezo chuo cha taifa cha utalii Arusha ambapo mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi za taifa (Tanapa) Allan Kijazi amesema Tanapa itahakikisha inakuwa chachu ya mpango huo wa kuboresha huduma za utalii.

Naye kaimu afisa mtendaji mkuu wa chuo cha utalii Arusha Bi Consada Msoma amesema chuo cha utalii kina mipango mizuri katika kuboresha huduma za utalii lakini kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha za kutosha katika kufanikisha malengo yake.
No comments