Angalia Picha za Mapokezi ya Diamond Platnumz Uwanja wa Ndege Dar Akitokea Marekani...
Tarehe 10/7/2014 ni siku
ambayo Star wa muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania Diamond Platnumz,
ambaye anachafua anga la muziki kwa sasa kwa utunzi na uimbaji wake
alitua katika Uwanja wa Ndege Mwal. Jurius Nyerere, mnamo mishare ya saa
nne na nusu za usiku akitokea nchini Marekani ambapo alikua huko
kushiriki katika Tuzo kubwa Dunia BET awards, ambazo hufanyika kila
mwaka, Diamond alikua katika kategori ya Best African Act ambayo
ilichukuliwa na Davido kutoka Nigeria.
Watanzania wenye moyo wa Upendo na Kizalendo walijitokeza katika
viwanja vya ndege kumpokea Msanii huyo, wakiwa na mabango makubwa kabisa
yenye maneno ya kuashiria ushujaa aliouonyesha Diamond katika muziki na
kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania katika muziki, Uwanja wa ndege
wa Mwl. Julius Nyerere, uligubikwa na Kelele za Furaha na Sauti
zilisikika zikiimba wimbo wa Mdogomdogo ikiwa ni mapenzi ya dhati kabisa
kwa Diamond kwa kutuwakilisha vema na kurejea salama, hakika kazi ya
muziki wetu kwa sasa inaonekana.
Diamond
baada ya kufika aliwashukuru wote waliofika kumpokea na kusema kuwa
safari yake ilikua nzuri na amejifunza vitu vingi sana pia amekutana na
watu wengi na tutaraji mengine mengi na mazuri katika muziki wetu, na
kwa upande mwingine alitoa shukran za dhati kabisa kwa watanzania
kuipokea vema video yake mpya ya mdogomdogo, imekua ikifanya vizuri sana
na hata youtube imekuwa na views wengi kwa muda mchache
No comments