Header Ads

CCM yatoa onyo kwa wanaotangaza nia ya kugombea Urais 2015 kwa tiketi ya chama hicho

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitawapima mwezi ujao Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe ili kujua ni kwa kiasi gani wametekeleza masharti yatokanayo na adhabu wanazotumikia kutokana na kukiuka kanuni na taratibu za chama hicho kwa kutangaza kabla ya wakati juu ya nia yao ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu 2015.

Makada wengine watakaopimwa kama Lowassa na Membe ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mawasiliano na Uratibu), Stephen Wassira na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, makada hao watapimwa na Kamati ya Usalama na Maadili ya CCM.

Nape alitangaza uamuzi huo jana wakati akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam.

Februari 18 mwaka huu, CC ya CCM ilitoa adhabu kwa makada hao, kila mmoja akitakiwa kutumikia adhabu hiyo kwa miezi 12. Mwezi ujao (Agosti), makada hao sita watakuwa wametimiza miezi sita.

Nape alisema baada ya wote kupimwa, ikiwa watabainika kuwa hawakutekeleza ipasavyo adhabu zao, yatatolewa maamuzi na kupendekeza CC kuwaongezea adhabu zaidi.

Aidha, Nape aliwatahadharisha baadhi ya wanachama walioonyesha nia ya kuomba ridhaa ya CCM ya kugombea urais kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za chama zinazosimamia masuala hayo ili wasipoteze sifa za kugombea.

Alisema hawatawavumilia wanachama wenye nia ya kukivuruga chama kwa kutoheshimu na kutozifuata kanuni na taratibu zake na kwamba, badala yake wataendelea kuwachukulia hatua.

“Ni muhimu wanachama wakakumbuka kwamba chama ni pamoja na katiba, kanuni na taratibu zake, hivyo kutoziheshimu na kutozifuata ni kukivuruga chama. Na tukisema tuwaache watavuruga chama, jambo ambalo halivumiliki,“ alisema Nape.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha chama kinabaki kuwa na umoja na mshikamano ambao ni muhimu, hasa kuelekea kukamilisha kazi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2010/15 pamoja na uchaguzi mkuu mwakani.

ADHABU ZA KINA LOWASSA, MEMBE
Makada hao (Lowassa, Membe, Wassira, Makamba, Ngeleja na Sumaye) walipewa adhabu Februari 18 mwaka huu ili wajirekebishe, hiyo ni baada ya kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Udhibiti na Tume ya Udhibiti na Nidhamu ya chama hicho.

Baada ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao zilikuwa za kweli na hivyo kupendekeza waadhibiwe.

Baadhi ya makosa waliyothibitika kutenda ni pamoja na kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea urais kabla ya wakati kinyume cha Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).

Kosa jingine ni kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010.

Baada ya kuthibitisha makosa hayo, CC ya CCM iliwapa adhabu ya onyo kali na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo, chama kitawachukulia hatua kali zaidi.

Adhabu hiyo, kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b), inamtaka

No comments

Powered by Blogger.