Baada ya shambulio la Pwani-Kenya baraza la Jamuhuri ya Mombasa (MRC) Lajengwa na vikosi vya usalama vya kenya
Baraza la Jamhuri ya Mombasa iliyojitenga (MRC)linajiunda tena katika mkoa wa Pwani wa Kenya, ambao umekuwa na mlolongo wa wasiwasi wa kisiasa na hali ya kukosekana kwa usalama baada ya mfululizo wa mashambulio yaliyofanywa na vikundi vyenye silaha mwezi uliopita, maofisa usalama wamesema.
Kamishna wa Kaunti ya Kilifi Albert Kobia alisema serikali ina ripoti muhimu ya upelelezi inayoonyesha kwamba MRC inajiunda tena na kuajiri wanachama wapya kwa ajili ya mafunzo ya kusababisha vurugu katika nchi.
"Wakaazi pia walituthibitishia kuona vikundi vya watu wakiingia na kutoka kwenye misitu katika maeneo hayo," aliiambia Sabahi. "Wakaazi pia walitujulisha kwamba kikundi cha watu wamekuwa wakipita kuuliza watu kujiunga na MRC kupambana kwa ajili ya haki za wakaazi wa Pwani."

Aidha, katika mapambano ya uvamizi ya tarehe 3 Julai, vikosi vya usalama viliwakamata washukiwa saba ambao ni wanachama wa MRC katika msitu wa Kaya Chonit, wakati wengine madazeni walikimbia, alisema. Polisi walipata silaha zilizopangwa ikiwa ni pamoja na bunduki zilizotengenezwa kienyeji, pinde na mishale, mapanga na mashoka.
"Tunawatafuta wale waliotoroka kwa kuwa tuna taarifa zinazowahusu baadhi yao," Kobia alisema. "Tangia kikundi hicho kilishughulikiwa katika kaunti ya Mombasa, wanachama wamejipanga tena katika vijiji vya ndani katika kaunti nyingine kwa matumaini kwamba shughuli zao hazitagundulika."
Historia ya makabiliano
Katika kufikia kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2013, serikali ilichukua hatua kali za kinidhamu kwa MRC, ambalo lilitishia kugomea uchaguzi katika mkoa wa Pwani.
Hatua hizo kali za kinidhamu zilisababisha mauaji ya wanachama kadhaa wa MRC na kukamata makumi ya wengine, ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa kikundi Omar Mwamnuadzi na msemaji Mohammed Rashid Mraja.
Wanachama hao waliachiwa kutoka jela kwa masharti kwamba watadumisha amani na kuacha wito wao wa kujitenga.
Hatahivyo, Kobia alisema, baadhi ya wanachama wa MRC kwa sasa wanafanya shughuli zao chini ya mitindo wa kujifanya marafiki na kusababisha vurugu dhidi ya wasio raia wa mkoa wa Pwani.
"Kwa msaada wa wakaazi, tumeweza kujua mipango ya MRC ya kusababisha machafuko wakati wa kufikia kilele cha mkusanyiko wa kisiasa wa tarehe 7 Julai. Tuko katika tahadhari kubwa siyo kuwapa nafasi ya kusababisha maangamizi," alisema, akiongezea kwamba "kikundi hicho kwa sasa kina ajenda ya kusababisha vurugu nchi nzima".
Kwa kukamatwa kwa wanaodaiwa kuwa wanachama wa MRC mwezi huu, maofisa hawahukumu tu uhusika unaowezekana wa kikundi hiki katika mashambulio ya Kaunti ya Lamu katika lengo lao la kukidhi ajenda yao, Kobia alisema.
Mchambuzi wa masuala ya usalama wa Kenya na mstaafu wa jeshi Meja Bashir Haji Abdullahi alisema wasiwasi wa kisiasa wa muda mrefu na kukosekana kwa hali ya usalama kwa ujumla nchini Kenya kunaweza kusaidia kikundi chochote kinachotafuta kusababisha vurugu katika nchi.
"Kushindwa kwa serikali kushughulikia vurugu za mara kwa mara na kuwatia hatiani wakosaji kunaweza kutia moyo kikundi chochote," aliiambia Sabahi. "kumekuwa na kukamatwa kwa washukiwa wanaotuhumiwa kuhusiana na mashambulio ya Kaunti ya Lamu, lakini kunaonekana kama mjibizo wa nguvu ya soda kunakofanywa na serikali kutuliza umma wasiopendezwa na hilo."
Ukamataji umechukua mwelekeo wa kisiasa na kidini na umeongeza hali ya machafuko iliyopo, ambayo kundi la wanamgambo wanaweza kuitumia, alisemaa.
Alisema serikali inapaswa kushughulikia baadhi ya malalamiko halali yaliyotolewa na MRC na watu wengine katika mkoa -- kama vile maendeleo ya kiuchumi, elimu na ujenzi wa miundombinu -- na kushughulikia kile kinachowezekana.
Aidha, Abdullahi alisema, MRC haikuvunjwa kabisa, bali inashughulikiwa tu katika kujaribu kuepuka mapigano na vikosi vya usalama.
"Kwanza kabisa MRC bado inafanya kazi kwa kuwa ni kundi lililosajiliwa," alisema. "Aidha, Mahakama Kuu ililipa kundi uhalali kwa kubadilisha maana ya serikali ya kundi kama kundi la kigaidi mwaka 2012."
MRC 'yasingiziwa' kwa kushindwa kwa serikali
Katibu Mkuu wa MRC Hamza Randu alisema madai ya serikali dhidi ya kundi hayana msingi.
"MRC ina makubaliano ya kudumisha amani na kuhusiana na kuhusika kwetu makubaliano hayo yamevunjwa," Randu aliiambia Sabahi. "Baadhi yetu tunafunga na hatuna muda au mipango ya kusababisha uharibifu kama serikali inavyodai."
"Serikali inataka kuutuliza umma [kwa kuonyesha] kwamba inafanya jambo katika usalama na MRC inasingiziwa kwa kushindwa kwa serikali kuwalinda watu wake," alisema. "Tuhuma hizi zinaweza pia kuwa hila ya serikali kujenga nadharia na Rais [Uhuru] Kenyatta kwamba [makundi ya kisiasa] ya wenyeji yanahusika."
Mchambuzi wa masuala ya usalama na kanali wa jeshi mstaafu Daud Sheikh Ahmed alisema tuhuma dhidi ya MRC zinaweza kuwa propaganda za serikali katika kujaribu kurejesha imani ya wananchi iliyopotea katika vyombo vya usalama.
Alisema tangu Kenyatta kuwaondoa al-Shabaab katika mashambulio huko Mpeketoni na miji mingine katika Kaunti ya Lamu, viongozi katika mkoa wa Pwani wamekuwa wakitoa tuhuma zisizothibitishwa dhidi ya MRC.
Tuhuma hizo zilizidishwa wakati Makamu wa Rais William Ruto alipotoa sharti la mwisho la saa 48 kwa ajili ya kukamatwa kwa wauaji katika mji wa Hindi, alisema.
"Kwa kuhofia kupoteza kazi zao, viongozi wa eneo wanailaumu MRC kwa kuzingatia vurugu zao ailizopita," Ahmed aliiambia Sabahi.
"Sheria ya Kenya inaeleza kwamba mtuhumiwa anapaswa kupelekwa mahakamani ndani ya saa 24 baada ya kukamatwa," alisema. "Lakini zaidi ya wiki mbili tangu walipowakamata watuhumiwa wa MRC huko Kilifi, hakuna ambaye amefikishwa mahakamani."
"Mamlaka za serikali zinatakiwa kuwa makini kwa tuhuma zake au propaganda zitawarudia," alisema

No comments