Mama amkimbia mwanae baada ya kuona kuwa ni mlemavu....
Mkazi wa Kata ya Magugu, Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, Stella Juma (43), anaomba wasamaria kusaidia matibabu na malezi ya mjukuu wake mwenye umri wa siku (24) aliyezaliwa akiwa na ulemavu kichwani.
Akizungumza na paparaziwetu, Bibi wa mtoto huyo, Stella Juma, amesema mtoto huyo alizaliwa April 27, 2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Meru, Patandi mkoani Arusha, na kuzaliwa ubongo wake ukiwa nje na mdomo ukiwa umepasuka hali inayomfanya aishi kwa shida.
Amesema kuwa hali hiyo iliyosababisha mama mzazi wa mtoto huyo, Tausi Khamis, kukataa kumnyonyesha mtoto wake wa kumzaa baada ya kumuona kuwa ana ulemavu huo na kukimbilia kusiko julikana.

Mtoto Charles Frank, ambaye amezaliwa ubongo wake ukiwa nje, msaada wako utaokoa maisha yake
Aidha amewaomba wasamaria wenye nia ya njema kumsaidia kupata fedha za matibatu katika Hospitali ya Rufaa ya Selian iliyopo jijini Arusha, kwani hawezi kumudu gharama hizo kutokana na Baba wa mtoto huyo kutokuwa na uwezo wa kupata fedha ambazo zinahitajika katika matibabu.
“Tulivyoenda Hospitali ya Seliani walituambia tumemchelewesha mtoto kumleta hospitalini, kwahiyo wametuambia tusubiri amalimize umri wa miezi mitatu ndipo atafanyiwa upasuaji lakini wametuambia tujiandae kwa gharama za upasuaji lakini sisi hatuna fedha kwahiyo tunaomba kupitia kwenu Watanzania watusaidie kupata mchango wa hali na mali ili kuokoa maisha ya mtoto japo kuwa hawajatuambia kiasi hadi atomize huo mda” alisema mzazi huyo.
Hata hivyo, amesema wasamaria wenye nia ya kumsaidia wanaweza kumchangia kupitia namba 0762684005 ili kufanikisha zoezi hilo, ambapo hali ya mtoto huyo kufikia leo jioni imezidi kuwa mbaya na kuwalazimu kumpeleka katika Hospitali ya Hydom iliyopo mkoani Manyara kutokana na hali yake kutoridhisha.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Hydom, Olav Espegren, alithibitisha kumpokea mtoto kuyo na kusema wauguzi na madaktari wa hospitali hiyo, wanaendelea kumpatia matibabu mtoto huyo pamoja na kukausha kidonda kilichopo kichwani mwake.
No comments