Wananchi kuwa makini.... Majani ya papai hayatibu homa ya Dengue....
Halmashauri ya manispaa ya Ilala imesema kuwa majani ya mapapai si tiba ya ugonjwa wa dengue hivyo ni vyema wananchi wakafika hospitalini kupatiwa dawa kuliko kudanganywa na waganga wa jadi....
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Ilala, Dr Willy Sango, wakati wakitoa mafunzo kwa wenyeviti wa serikali za mitaa jinsi ya kuelimisha wananchi jinsi ya kujikinga na homa ya dengue...
Dr Sango alisema ugonjwa wa dengue hauna tiba wala chanjo bali wanatibu dalili za ugonjwa huo tu, hivyo ni vyema wananchi wakachukua tahadhari ya kujikinga nao....

Pia aliwataka waganga wa jadi kuacha kuwadanganya wananchi kwa kusema kuwa majani ya papai yanatibu kwani hiyo si kweli na hayajathibitishwa na wataalam wa afya...
Alisema kuwa mtu akiugua anatakiwa aende hospitali kwanza, asiende kutumia dawa bila kupima kwani hiyo ni hatari, hivyo wananchi wanatakiwa kufika hospitalini kupima ndipo waanze kutumia dawa....
Hata hivyo alisema, wenyeviti wa serikali za mitaa wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia vizuri maeneo yao pamoja na kushauri wananchi kwenda hospitali na kuacha kudanganywa na majani ya mapapai....
"Majani ya papai si dawa ya dengue wala hayajathibitishwa na mpaka sasa hakuna dawa ya ugonjwa huo. Tunacho tibu ni dalili zake tu, hivyo wananchi msidanganyike na waganga wachache wanaotaka pesa," alisema Dr Sango
Pia alisema kuanzia kesho, dawa zitaanza kupuliziwa mtaa mmoja baada ya mwingine ili kuua mazalia ya mbu hao wanaoeneza ugonjwa huo....
Hata hivyo alisema kuwa watu wanaopulizia dawa hizo wanatakiwa kufika katika ofisi za serikali za mitaa ili watambuliwe kwanza ndipo waendelee na zoezi hilo.

No comments