Header Ads

Kijana afungwa jela miaka 6 kwa kosa la kumchoma dada yake kisu cha Titi.....

Mkazi wa mtaa wa Katoma mjini Geita Paul Kakwaya(43) amehukumiwa kwenda jela miaka sita na kulipa faini ya shilingi 1,000,000= kwa kosa la kumchoma kisu dada yake Koleta Kakwaya(78) mkazi wa mtaa huo.

Awali mwendesha mashitaka wa serikali Ester Magoti ameieleza Mahakama ya wilaya ya Geita kuwa usiku wa Aprili 18 mwaka huu Kakwaya alienda nyumbani kwa Koleta na baadaye alimshambulia Koleta kwa kumchoma kisu kifuani.

Magoti ameifafanualia mahakama kuwa, Kakwaya alimkaba shingo Koleta na kumchoma kisu sehemu ya ziwa la kushoto, huku akikivuta kuelekea ziwa upande wa kulia kabla ya kumvutia chumbani na yeye Kakwaya akabaki amelala sebuleni.
Amesema kelele za Koleta kuomba msaada zilisikika, na majirani walipofika walimkuta Kakwaya amelala sebuleni akionekana mithili ya mtu aliyechanganyikiwa, huku Koleta akiwa chumbani na kisu kikiwa kimenasa kifuani, kabla ya kumpeleka hospitalini kwa matibabu.

Hali ya Koreta bado ni mbaya hospitalini hapo kwani hajiwezi hata kuongea, hatua iliyosababisha kesi hiyo kusikilizwa bila ushahidi wake, ingawaje mahakama imedai ushahidi uliotolewa kwenye kesi hiyo umejitosheleza.

Hakimu wa mahakama hiyo Zabloni Kesase amesema ushaidi wa pande zote umedhihirisha Kakwaya amepatikana na hatia, hivyo atatumikia Kifungo cha Miaka Sita Jela, na Kulipa Faini ya shilingi 1,000,000= ili liwe fundisho kwa jamii.

No comments

Powered by Blogger.