Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya vurugu za waendesha bodaboda mbeya....
Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara pikipiki maarufu kama bodaboda mara baada ya waendesha bodaboda hao kufunga barabara kushinikiza kutaka nkuchukua sheria mkononi kwa mtuhumiwa aliyedaiwa kumuuwa muendesha bodaboda Mwenzao. Wakieleza zaidi wamesema kwamba Juzi kuna muendesha pikipiki mmoja alitekwa na kisha kuuuliwa na mtu/watu wasiofahamika ambapo jana alizikwa.
Leo Asubuhi waendesha bodaboda hao kupata taarifa kuwa Mtu aliyefanya mauwaji hayo ameonekana mtaani ndipo walipoandamana kwenda kumkamata mtuhumiwa huyo wakati huo jeshi la Polisi walishapata taarifa kuhusu tukio hilo na kuwahi eneo latukio walipofika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa huyo hali iliyosababisha mtafaruku waendesha bodaboda hao kushinikiza Jeshi la Polisi kuwakabidhi mtuhumiwa aliyehusika na mauwaji ya mwenzao hali iliyoleta vurugu ndipo jeshi la Polisi walipolazimika Kutumia Mabomu ya Machozi kuwatawanya.
No comments