Baby Madaha ajibu mapigo ya mwenyekiti wa Bongo Movie,Steve Nyerere....
Nyemo Chilongani VITA ni vita! Mwanadashosti anayesukuma maisha laifu kupitia filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha amesema anamshangaa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ kwa kauli aliyoitoa dhidi yake kuwa hayupo sehemu yoyote ile.
Akifafanua kuhusiana na kauli hiyo aliyoitoa mwenyekiti huyo wiki iliyopita, Baby alijibu mapigo kuwa kiongozi huyo alipotosha umma kwani yeye ni memba halali wa Bongo Movie Unity.
“Steve anasema hajui nipo wapi, hivi ni kweli mwenyekiti hawajui watu waliokuwa na kadi ya uanachama? Mimi nipo kotekote, nipo Bongo Movie, nipo hata Bongo Fleva, kama akitaka kadi aseme nimwoneshe, sionekani sana kwani muda mwingi nakuwa Kenya,” alisema Baby Madaha, alipotafutwa Steve, hakuwa tayari kufafanua ishu hiyo.Akifafanua kuhusiana na kauli hiyo aliyoitoa mwenyekiti huyo wiki iliyopita, Baby alijibu mapigo kuwa kiongozi huyo alipotosha umma kwani yeye ni memba halali wa Bongo Movie Unity.
No comments