Header Ads

Mkurugenzi wa Msama Promotion amepata ajali mbaya iliyohusisha bodaboda......

Mkurugenzi wa Msama Promotions, Bw Alex Msama amepata ajali mbaya eneo la ipagala Mwisho muda mfupi uliopita na Katika ajali hiyo iliyohusisha Mwendesha Bodaboda na gari ya Mr Alex Msama.

Baada ya ajali hiyo kutokea Waliweza kukimbizwa Katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Kwa matibabu zaidi na wameweza kupatiwa matibabu na kupelekwa katika Chumba cha X-ray na mpaka paparaziwetu anaondoka Hospitali hapo majibu ya x-ray yalikuwa bado hayajatoka lakini hali zao sio mbaya sana.

Katika ajali hiyo iliyohusisha gari na bodaboda hakuna aliyepoteza maisha. Bw Msama amepata majeraha madogo madogo sehemu za mikononi lakini pia na kusikia maumivu katika kifua. Huku mwendesha bodaboda nae hali yake sio mbaya sana japokuwa ana maumivu katika sehemu mbalimbali za mwili na wagonjwa wote wanaendelea na kupewa matibabu katika hospitali ya Mkoa Dodoma.



Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

No comments

Powered by Blogger.