Arsenal yaifunga Everton 4- 1
MSHAMBULIAJI
Olivier Giroud ametokea benchi na kufunga mabao mawili Arsenal
ikiifunga Everton 4-1 na kujitengenezea mazingira ya kutinga Nusu
Fainali za Kombe la Uwanja wa Wembley.
The
Gunners walikuwa tayari mbele ndani ya dakika saba wakati Mesut Ozil
alipojisafisha mbele ya mashabiki kwa kumtungua kipa wa Everton, Joel
Robles.
Pamoja
na hayo, Everton ikasawazisha kwa shambulizi la kushitukiza la Ross
Barkley aliyempasia mfungaji Romelu Lukaku dakika ya 32.
Arsenal
- ambayo inatakiwa kuifunga Bayern Munich wiki ijayo kukipiku kipigo
cha 2-0 walichofungwa kwenye mechi ya kwanza ya Hatua ya 16 Bora Ligi ya
Mabingwa Ulaya, ilipata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo wa zamani wa
Everton, Mikel Arteta aliyefunga kwa penalti dakika ya 67. Giroud
alifunga dakika ya 83 na 85 baada ya kuingia dakika ya 60 kuchukua
nafasi ya Sanogo
Tumewanyamazisha: Olivier Giroud akimuinua Mesut Ozil juu baada ya kufungia Arsenal bao la nne
Giroud akifunga moja ya mabao yake leo
TUNAOMBA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSU TAARIFA HII!!!
TUNAOMBA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSU TAARIFA HII!!!
No comments