ANGALIA PICHA CHADEMA (M4C PAMOJA DAIMA) YATETEMESHA MWANZA
Wananchi
wa Jiji la Mwanza wakiwa wameinua mikono kuonesha ishara ya Kusurrender
katika Mkutano wa hitimisho wa Chadema M4C Pamoja Daima ulifanyika
katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza
Helkopta
iliyokuwa imembeba Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Wilbroad Slaa ikitua
katika Uwanja wa Furahisha ili aweze kuhutubia katika Mkutano wa Kampeni
wa Chadema M4C Pamoja Daima.
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akiingia Uwanjani ili aweze kuhutubia maelfu wa Wana Mwanza waliofika Kumsikiliza.
Mbunge wa
Musoma mjini, Vincent Nyerere akihutubia katika Mkutano wa hitimisho wa
M4C Pamoja Daima lillofanyika katika viwanja vya Furahisha Jijini
Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Highness Kiwia akitoa ya moyoni katika Mkutano wa Movement For Change Pamoja Daima.
Mh. Higness
Kiwia akimpokea Bwana Darius Ngoko ambaye ameamua kuhama chama cha
Mapinduzi CCM na Kujiunga na Chadema katika Mkutano wa M4C Pamoja Daima.
Katika hali ya kushangaza jeneza ambalo lilikuwa limechorwa picha ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe.
Bwana
Kaswahili aliyevaa shati la blue kamanda kutoka chama cha Chadema ambae
anajiandaa kugombea katika Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema
akifuatilia kinachoendelea katika Mkutano huo.
Katibu
wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Bwana Laban Aggrey naye akifuatilia kwa
umakini matukio kadha wa kadha katika Mkutano wa M4C Pamoja Daima akiwa
na baadhi Makamanda wa Chadema.
Mkurugenzi
wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo Chadema Bwana
Wilfred Mganyizi Lwakatare akizungumza kwenye mkutano wa M4C Pamoja
Daima katika viwanja vya Furahisha.
Mdhamini wa Chadema Mzee Masinde akizungumza jambo katika Mkutano wa M4C Pamoja Daima katika viwanja vya Furahisha.
Mbunge
wa Nyamagana, Mh. Ezekia Wenje akiwa na Matibu wa Chadema Taifa Bwan
Mudi mwenye kombati ya Green na Mbungue wa Jimbo la Ilemela Mh. Highness
Kiwia.
Umati wa watu wakiwa wamekaa wakisikiliza hotuba kutoka kwa Dr. Wilbroad Slaa kama inavyoonekana katika picha.
Umati
mkubwa wa wananchi waliofika kwenye uwanjaa wa Furahishaaa wakisikiliza
hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi wa Chadema kwenye Kampeni ya M4C
Pamoja Daimaa.
Katibu
wa Chadema Taifa, Dr. Wilbroad Slaa akihuthubia maelfu ya wananchi
waliofurika katika uwanja wa Furahisha Mwanza kusikiliza hitimisho la
Kampuni ya M4C Pamoja Daima.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimesema hakitalalamika
tena kwa lolote au kukilamu Chama Cha Mapinduzi CCM maana wameshaongea
sana na sasa watafanya utekelezaji wa Ilani ya Chama chao.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Chama hicho Dr. Wilbroad Slaa katika
hitimisho la Kampeni za M4C Pamoja Daima lililofanyika katika uwanja wa
Furahisha Mwanza.
Slaa amesema kuwa wameshaongea kero mbalimbali za wanainchi wa
Tanzania lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika hicho wao kuanzia sasa
wao kama Chadema hawatalalamika zaidi ya kuchukua maamuzi ya utekelezaji
tu.
Kampeni hizo ambazo imefanyika kwa siku 14 kwa kutembelea Majimbo
yote ya upigaji kura ambazo zilikua zimegawanyika katika makundi mawili
kwa kutumia helkopta tatu ambazo zilikuwa zinaongozwa na Dr. Wilbroad
Slaa, Freeman Mbowe na Tundu Lissu.
No comments