Header Ads

WAZIRI WA MAWASILIANO SAYANSI NA TECHNOLOJIA AHIMIZA VYUO VYA UFUNDI KUZALISHA WATAALAMU

Dar es Saaam. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa,amevitaka vyuo vya ufundi kuhakikisha vinawaandaa wataalamu ili nchi ijiendesha kwa viwanda, hasa kwa wakati huu ambapo rasilimali nyingi zinagundulika kama vile gesi, mafuta na madini .Mbarawa aliyasema hayo jana, alipohudhuria mahafali ya saba ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, ambapo aliwatunuku wahitimu wa fani mbalimbali waliohitimu mafunzo yao chuoni hapo.Alisema nchi inayotaka kupata maendeleo ya haraka, inawekeza kwenye fani za Sayansi na Teknolojia, huku akiitaka taasisi hiyo kuwa ni ya mfano wa kuigwa kwa kuwaandaa vijana walio mahiri kwenye fani husika na wenye moyo wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

Alifafanua kuwa, nchi zenye maendeleo makubwa duniani ni zile zinazowekeza katika Elimu ya Ufundi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano akitolea mfano nchi zilizoendelea kiviwanda, alizodai zimepata mafanikio kwa kuwekeza kwenye sekta ya viwanda na ufundi.
"Hivi sasa Taifa letu linahimiza na kutafuta wawekezaji katika rasilimali za gesi, mafuta na madini. Haya ni maeneo yanayohitaji ufundi mkubwa ili kuweza kutumia vyema na kunufaisha watu wetu na taifa kwa jumla," alisema Mbarawa.
Serikali ili kuboresha maisha ya Watanzania,inahitaji wataalamu watakaosimamia ujenzi wa reli, barabara, bandari na viwanja vya ndege.

No comments

Powered by Blogger.