Header Ads

MFANYABIASHARA WA SIMU APIGWA RISASI HUKO MBEYA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi   

Taarifa zilitufikia, zinasema kuwa, mfanyabiashara wa simu eneo la Ilomba Jijini Mbeya, amepigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo, alipokuwa akielekea nyumbani kwake.
 
Imeelezwa kuwa alitoka dukani kwake ambako anauza simu akielekea nyumbani kwake eneo la Isyesye Nanenane, ndipo alipovamiwa na watu hao kisha kumpiga risasi ya mguuni na kumpora fedha na gari lake na sasa amelezwa hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu.
 
Jeshi la polisi mkoani Mbeya, linaendelea kuwasaka watu hao.

No comments

Powered by Blogger.