CHADEMA WAIOMBA MAHAKAMA KUTUPILIA MBALI KESI YA ZITTO..
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeomba Mahakama kutupilia mbali
kesi ya madai, iliyofunguliwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama
hicho, Zitto Kabwe dhidi yao kwa kuwa haina msingi kisheria. Walidai
hayo katika pingamizi la awali, walilowasilisha juzi katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, kupitia kwa mawakili wao, Peter Kibatala na
Tundu Lissu.
Katika
pingamizi lao, Chadema wanadai shauri halina msingi kwa kuwa
halikufunguliwa katika Mahakama za chini zenye mamlaka ya kusikiliza na
kutoa uamuzi kwa mujibu wa Sheria za mwenendo wa kesi za madai.
Kwa
mujibu wa hati ya pingamizi hilo, Zitto anaendesha mashauri mawili dhidi
ya Kamati Kuu ya Chadema kwa wakati mmoja, jambo ambalo ni matumizi
mabaya ya Mahakama.
Wanadai,
kesi hiyo imewasilishwa kwenye masijala Kuu ya Mahakama Kuu badala ya
masijala ya Wilaya kinyume na taratibu za masijala za Mahakama na pia
hajaomba maoni ya Mahakama Kuu kuhusu suala lake la uanachama.
Aidha,
wanadai Mahakama Kuu siyo sehemu ya kushughulikia suala lake, bali Zitto
alitakiwa kutumia nafasi nyingine zilizo ndani ya chama. Wanadai
Mahakama haina mamlaka ya kutoa uamuzi wa ombi lake kwa Chadema
kutoingilia uanachama wala ubunge wake, kwa kuwa itakuwa inaingilia
mamlaka ya vyama vya siasa katika kuwaadhibu wanachama wake.
Zitto
ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini amefungua kesi ya madai dhidi ya
Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Dk Willbrod Slaa.
Katika
kesi hiyo, anaiomba Mahakama itoe zuio kwa Kamati Kuu au chombo chochote
ndani ya chama, kujadili suala la uanachama wake, hadi atakapokata
rufaa ya kupinga uamuzi uliomvua uongozi wa chama.
Zitto
anaiomba Mahakama imwamuru Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa ampe nakala
zinazotoa sababu za uamuzi wa kumvua uongozi katika kikao kilichofanyika
Novemba 22 mwaka jana, ili akate rufaa katika Baraza Kuu la Chama.
Aidha
anaomba Mahakama iamuru Chadema isiingilie kazi zake za ubunge wala
uanachama wake. Kesi hiyo namba moja ya mwaka huu itatajwa Februari 13
mwaka huu mbele ya Jaji John Utamwa.
Tayari
Mahakama imetoa amri kwa Kamati Kuu ya chama hicho au chombo chochote
cha Chadema, kutojadili suala la uanachama wa Zitto hadi kesi yake ya
msingi aliyoifungua mahakamani, itakaposikilizwa.
Katika
uamuzi wake, Jaji Utamwa alisema Zitto amekidhi matakwa ya kisheria, kwa
kuwa zuio hilo lisipotolewa na akavuliwa uanachama bila kusikilizwa,
atapoteza nafasi ya ubunge na kushindwa kuwatumikia wananchi
waliomchagua ; na pia atap
No comments