ANGALIA PICHA YA MATESO ANAYOPATA KIJANA HUYU
Shaggy Sadick mwenye umri wa miaka 18
MATESO kila
kukicha. Kijana Shaggy Sadick mwenye umri wa miaka 18, mkazi wa Musoma
mjini, Mkoa wa Mara yuko katika mateso makubwa baada ya tumbo lake
kuvimba na kuongezeka ukubwa hali inayomfanya ashindwe kutembea.
Akizungumza
kwa masikitiko makubwa, dada wa Shaggy, Mariam Sadick, alisema mdogo
wake alianza kuumwa ugonjwa huo tokea akiwa na umri wa miaka 12 na kwa
muda wote huo, wamehangaika katika hospitali mbalimbali nchini bila
mafanikio.
Alisema
awali walianza kumpeleka katika Hospitali ya Musoma na baadaye Bugando
jijini Mwanza ambako baada ya vipimo, iligundulika kwamba alikuwa
akisumbuliwa na tatizo la moyo ambao umejaa maji, ugonjwa ambao anapaswa
kutibiwa nje ya nchi ili kuumaliza.
“Kwa
kweli tumehangaika naye sana kumsaidia apone, lakini imeshindikana
kwani ili apone, wanapaswa kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu, kitu
kinachotishia uhai wake kwani familia ni duni,” alisema dada huyo.
Dada
huyo alizidi kulia kwa kusema kwamba kingine kinachomsikitisha ni
kwamba mdogo wake amekosa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu
kwani kwa matatizo aliyonayo, hawezi kutembea tumbo limefika hadi
magotini.
Alisema
wakati wa kulala ukifika, mdogo wake hupata wakati mgumu kwani
wanalazimika kumuwekea mito mingi ya kulalia nyuma yake, vinginevyo
anaweza kupoteza maisha kwa sababu ya kushindwa kupumua vizuri.
“Kwa
kweli kitu ambacho kinatusikitisha wote ni kukosa kufanya mtihani wa
kidato cha nne, maana hawezi kutembea tena wakati wa kulala ndiyo kama
hivyo,” alisema.
Mtoto
Shaggy yupo katika mateso makali sana, anahitaji msaada wa hali na mali
ili aweze kuyaokoa maisha yake ili apate matibabu, endapo utaguswa na
habari yake,kwa msaada wasiliana kwa namba
0713 612
533.CHANZO GPL
No comments