Serikali Imewaonya Walimu na Wanafunzi Nchini Kuepuka Udanganyifu Mtihani wa Kidato cha 4
WAKATI wanafunzi wa kidato cha nne wakianza mitihani yao leo, Serikali imewaonya walimu na wanafunzi nchini kuepukana na vitendo vya udanganyifu, ikiwa ni pamoja na kuficha majibu chooni.
Onyo hilo lilitolewa jana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, alipotembelea shule mbalimbali za manispaa ya Dodoma, kuangalia maandalizi ya mitihani hiyo.
Shule alizozitembelea ni Shule ya Sekondari Jamhuri, Kiwanja cha Ndege na Msalato.
Akizungumza na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo alisema katika mtihani huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia mtihani wa darasa la saba ambapo kulijitokeza tukio la mwalimu kujificha chooni kuwasaidia wanafunzi.
“Naomba nionye shule zote nchini ambazo zimejipanga kufanya udanganyifu kuacha mara moja kwa kuwa hatua hiyo itazipotezea thamani,”alisema Jafo.
Aliwataka walimu wasithubutu kufanya udanganyifu wowote na kuziingiza shule zao kwenye kashfa.
Jafo alisema mara nyingi mitihani hiyo inapofanyika kumekuwa na wizi na kutofuatwa kwa taratibu za mitihani.
“Kuna shule saa hizi zimejipanga kufanya udanganyifu ili wanafunzi wakafanye vizuri na kuonekana ni bora, nataka niwaambie ni vyema mkajiandaa vizuri na kuepukana na vitendo hivyo,”alisema naibu Waziri huyo.
Akizungumza na wanafunzi, Jafo aliwataka kujiepusha na vitendo hivyo kwa kuwa vitawafanya wafutiwe mitihani na kupoteza malengo yao kwenye maisha.
Wakati huo huo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amewahakikishia walimu kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia na kuwataka kuwajibika ipasavyo.
“Serikali imejipanga kuweka mambo sawa kwenye sekta ya elimu," alisema. "Tuvumilieni,tupo kwenye kipindi cha mpito."
"Wajibikeni kwa kuonyesha thamani kwenye kazi yenu.”