Picha: Safari ya Mwisho ya Simba Asiyefugika,Thomas Mashali Jijini Dar
Hatimaye mwili wa bondia Thomas Mashali umezikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
Mashali alifariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Hadi anafariki dunia, Mashali alikuwa ni bondia namba mbili kwa viwango baada ya Francis Cheka lakini ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kumtwanga Cheka.
Alikuwa na mikanda minne ya ubingwa katika mashirikisho mbalimbali likiwemo lile la UBO.
Mashabiki wengi walijitokeza kumuaga kwenye Viwanja vya Leaders kabla ya kumzika kwenye makaburi hayo ya Kinondoni.