Lowassa na Sumaye Wazua Jambo Bungeni
Mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye jana waliibua hamasa wa aina yake mjini hapa wakati walipotinga bungeni kwa mara ya kwanza tangu wajiondoe CCM na kujiunga na Chadema.
Lakini hawakuwa kwenye kiti cha Waziri Mkuu wala wabunge, bali juu ghorofani kwenye eneo la wageni mashuhuri bungeni.
Kiti cha Spika nacho kilikuwa tofauti. Spika Job Ndugai na naibu wake, Dk Ackson Tulia walikuwepo maeneo ya Bunge, lakini aliyeongoza alikuwa ni Najma Gina, ambaye ni mwenyekiti, kitu ambacho si kawaida.
Lowassa, ambaye aligombea urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita akipeperusha bendera ya Chadema na vyama vingine vitatu vya upinzani, aliingia bungeni kwa mara ya kwanza tangu Bunge la Kumi livunjwe Julai mwaka jana, wakati Sumaye, aliyekuwa Waziri Mkuu kwa miaka kumi wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, amekuwa nje ya chombo hicho kwa zaidi ya miaka kumi.