Ofisi ya Bunge, TCRA Kuburuzwa TAKUKURU kwa Tuhuma za Rushwa
Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), imeifikisha Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kutokana na harufu ya rushwa kwenye ununuzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Dk Matern Lumbaga, alisema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa Mamlaka hiyo, kwenye ofisi, taasisi na mashirika ya umma 70 kati ya 506.
Kwa mujibu wa Dk Lumbaga, katika ukaguzi huo wa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16, taasisi tisa za umma, ikiwamo Ofisi ya Bunge na wizara moja, zilibainika kuwa na viashiria vya rushwa.

Taasisi zingine mbali na Bunge ambazo nazo zimepelekwa Takukuru ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Makumbusho ya Taifa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Zingine ni Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Darts), Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
“Lengo la ukaguzi huo ni kuangalia kama ununuzi ulizingatia matakwa ya Sheria ya Ununuzi ya mwaka 2011 na mikataba ya ununuzi iliyoingia katika kipindi hicho.
“Kati ya taasisi za umma 506, ni taasisi 70 pekee ndizo zilifanyiwa ukaguzi kati ya Aprili na Septemba, ambapo taasisi 15 zimewekwa kwenye kundi la wizara, idara na wakala wa Serikali, mamlaka ya Serikali za Mitaa 25 na mashirika ya umma 30,” alisema.
Alisema pia mikataba 21,313 yenye thamani ya Sh trilioni 1.05 ilifanyiwa ukaguzi na kati ya hiyo, 845 ilihusu kazi za ujenzi; 7,179 vifaa na bidhaa; 103 ushauri wa kitaalamu; 3,083 ununuzi na mikataba na 453 makubaliano maalumu.
Dk Lumbanga alisema uchambuzi wa matokeo hayo ulionesha kuwa taasisi 22 zilikidhi viwango, 38 kiwango cha kati na 10 kiwango kisichoridhisha yaani chini ya asilimia
60.
Katika ukaguzi huo, walibaini malipo tata ya Sh. bilioni 1.32 kutoka kwenye taasisi nne kwenda kwa wakandarasi kwa kazi ambazo hazijafanyika.
Alitaja taasisi hizo kuwa ni Jiji la Dar es Salaam, Rea, Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk Laurent Shirima alisema wakati wowote Bodi ya Wakurugenzi itaita wakuu wa taasisi zilizofanya vibaya, wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua kutokana na uzembe na kuisababishia Serikali hasara.
Alisema pia kwa taasisi zilizopata chini ya asilimia 78, Mamlaka hiyo itaandaa utaratibu wa kuwapa mafunzo ya uelewa wa matumizi ya Sheria ya Ununuzi na kanuni zake.
“Ingekuwa rahisi kubaini upungufu iwapo taasisi zote zingewasilisha taarifa zao PPRA kwa wakati,” alisema.

No comments