Header Ads

Hivi ndivyo mapacha wa Shija wanavyowachanganya mabwana zao...

Kutokana na kufanana sura na maumbo waigizaji wa filamu Bongo ambao ni mapacha, Christina Mroni na Regina Mroni ‘Mapacha wa Shija’ wamewaweka katika wakati mgumu marafiki zao wa kiume baada ya kuwachanganya wasijue nani ni nani.

Mmoja wa mapacha hao, Christina alisema wanaume wao wamekuwa wakichanganyikiwa kutokana na kufanana kwao kwani hivi karibuni alikwenda ofisini kwa pacha mwenzake, lakini shemeji yake alipofika hapo alitaka kumkumbatia kimahaba akiamini ni mpenzi wake ambapo alilazimika kumkwepa.
“Mwenzangu alikataa na kukimbia akimwambia kwamba siyo yeye ndipo nikamwambia mimi ndiye mpenzi wake, akabaki ameduwaa, Mungu ni wa ajabu sana kwani hata watoto wetu ni wa kiume na wamepishana miezi miwili tu, nao wanafanana, tuna malengo ya siku zijazo tuwe  mapacha maarufu duniani,”alisema pacha huyo ambaye pamoja na mwenzake wameandaa filamu yao mpya inayoitwa Dada.

No comments

Powered by Blogger.