Header Ads

Breaking News: Lowassa atangaza rasmi kuhamia CHADEMA.....Asema CCM siyo Baba wala Mama yake, wananchi jitokezeni kujiandikisha ili kuing'oa CCM madarakani

Waziri  mkuu wa  zamani  Edward  Lowassa  ametangaza  rasmi  kukihama  chama  cha  mapinduzi, CCM mchana  huu  na  kutangaza  kuhamia  CHADEMA.....

 Lowassa  ametoa  kauli hii Bahari  Beach , Dar akiwa  sambamba  na  viongozi  mbalimbali  wa  UKAWA   ambao  wamekutana  na  waandishi  wa habari  kuzungumzia  hatima  yake  kuelekea  ikulu  pamoja  na  mapungufu  yaliyojitokeza  wakati  wa  mchakato  wa  kumpata  mgombea  urais  wa  CCM.


Lowassa  amesema  baada ya  kutafakari  kwa  kina  na  kujiridhisha, ameamua  kujiondoa  CCM kwa  kuwa  siyo  baba  yake  wala  mama  yake  na  kuitikia  wito  wa  UKAWA  kupitia  CHADEMA.

 Amesema  safari  yake  haitafanikiwa  iwapo  hawatajitokeza  watu  wengi  kupiga  kura na  anaiomba  tume  ya  uchaguzi  iongeze  muda  ili  watu  wote  waweze  kujiandikisha

Lowassa  amesema  alinyimwa  haki  yake  na  CCM  kama  mtanzania  kujieleza  na  kujitetea, hivyo  atakuwa  mnafiki  akisema  anaimani  na  chama  hicho.
Baada  ya  maelezo  hayo; Mwenyekiti  wa  CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe  alisimama  na  kumkabidhi  rasmi  Lowassa  Kadi  ya  CHADEMA.

No comments

Powered by Blogger.