Wema Sepetu akutana na mume wa Jay dee,Gadner!
Muigizaji maarufu nchini Wema Sepetu na Mchekeshaji MC Pilipili wanatarajiwa kuwa wa kwanza kukizindua kipindi cha Kili Chat Shows kinachotarajiwa kuanza leo. Kipindi hicho kitakachokuwa kikiendeshwa na Gadner G Habash kitakuwa ni cha nusu saa na kitakuwa kikiwakutanisha mastaa wawili wanaoshabikia timu za Yanga na Simba ambapo watapata nafasi ya kushindana namna wanavyozielewa klabu hizo.
Pia mashabiki watapata nafasi ya kuwahoji maswali kuhusu shughuli zao.Kipindi hicho kitakachokuwa kikirushwa Alhamisi saa tatu usiku katika kituo cha East Africa TV ni wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi huu kwa mashabiki wa Yanga na Simba kushiriki kampeni hiyo ambayo jumla ya Sh 100 zinashindaniwa kwa mashabiki kupiga kura kwa SMS kwa kutuma namba za ndani ya kizibo kila wanapokunywa bia ya Kilimanjaro.
No comments