Majambazi yapora fedha na kuua nje ya kiwanda cha viatu cha bora
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamepora begi linalodaiwa kuwa na fedha kisha kumpiga risasi ya shingo mwendesha boda boda na kupora pikipiki yake nje ya Kiwanda cha Bora, barabara ya Nyerere Dar es Salaam.
Father Kidevu Blog ilifika eneo la tukio na kukuta watu wakielezea tukio hilo na kulifananisha na la sinema kutokana na kile walichokiona.
Father Kidevu Blog ilifika eneo la tukio na kukuta watu wakielezea tukio hilo na kulifananisha na la sinema kutokana na kile walichokiona.
"Tuliona mzee mmoja tunahisi ni mfakazi wa Bora, alifika na pikipiki hapa, wakati anataka kuingia ndani wakafika watu wengine wawili katika pikipiki na kuamuru kupewa begi lile na ghafla mwenda pikipiki akawa anawahoji inakuaje wanachukua begi hilo ndipo tukasikia mlio wa risasi na bodaboda yule akaanguka chini wakamsukuma na kuchukua pikipiki yake na kukimbia nayo," alisema shuhuda yule.
Polisi ilifika eneo la tukio huku wengine wakiendelea na msako mkali dhidi ya wahalifu hao wakutumia sihala huku hofu ya kijana yule wa boda boda kupoteza maisha ikiwa kubwa kutokana na eneo alilopigwa risasi.
Baadhi ya Polisi wa doria ya Pikipiki wakiwa nje ya kiwanda cha Bora.
No comments