Ajali mbaya yatokea ikisababishwa na Abiria ....
Watu wasiozidi 50 wamenusurika kifo baada ya basi dogo kupinduka katika eneo la Sinai nje kidogo ya mji wa Songea mkoani Ruvuma kutokana na uzembe wa abiria .Ajali hiyo ilisababisha na mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni askari wa jeshi la kujenga Taifa JKT Mlale Songea ambaye alikuwa ni mmoja wa abiria kuamua kuendesha basi hilo baada ya dereva wa basi kutelemka na kumsaidia dereva mwenzake ambaye basi lake lilikuwa limeharibika.
Dereva wa basi lililopata ajali Bernad Bernad maarufu kwa jina la Kichefuchefu alisema yeye baada ya kutelemka kwenda kumsaidia dereva mwenzake alishangaa kuona gari lake linarudi nyuma likiendesha na mmoja wa abiria kisha kupinduka baada ya abiria huyo anayedaiwa kuwa ni mwanajeshi kushindwa kulimudu kuendesha .

“ Baada ya kutelemka nilishangaa kuona gari yangu inarudi nyuma kwa kasi kisha ikaanguka ikiwa na abiria ambao walipata majeraha na kukimbizwa katika hospitali ya Peramiho,mtu aliyesababisha ajali anayedaiwa kuwa ni askari wa JKT Mlale mara baada ya ajali amekimbia msituni tulijaribu kumkimbiza tumeshindwa kumkamata’’,alisema Bernad.
Hata hivyo mwandishi wakati anapita katika eneo la ajali hakuweza kukuta mtu yeyote aliyekuwepo kwenye ajali hiyo zaidi ya dereva wa basi hilo,utingo na wapita njia ambao walitoa lawama kwa askari huyo aliyeamua kuendesha gari wakati yeye alikuwa ni abiria na kusababisha ajali kwa uzembe.
No comments