Header Ads

Vijana ugumu wa maisha usitufanye tupoteze zawadi ya uhai tuliyonayo.... soma zaidi hapa

Kibaka mmoja apokea kichapo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali ni baada ya kumkwapua abiria mmoja mzigo wake ambao kwa haraka haukuweza kufahamika nini alitaka kuiba.
Kutokana na hasira za watu hao walioamua kujichukulia sheria mkononi,sidhani kama alipona kwani baadaye walitokea mgambo wa jiji na kumuokoa, Wakati wakielekea katika kituo cha Polisi cha Karume Kibaka huyo alianguka na kupoteza fahamu kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi kichwani.
Mmoja wa wananchi mwenye hasira kali akimponda na tofari Kibaka ambaye jina lake halikujulikana mara moja baada ya kudaiwa kumkwapua abiria mmoja aliyekuwa ndani ya gari akisafiri kuelekea Mwenge akiwa ametokea Tandika.
Kibaka huyo inadaiwa alimkwapua simu abiria huyo na kukimbilia katika eneo la makaburi yaliyopo Karume na ndipo lilipoibuka kundi la Watu na kuanza kumfukuza na hatimaye kufanikiwa kumkamata na kuanza kumshushia kibano cha nguvu kama uonavyo pichani.

No comments

Powered by Blogger.